Wednesday , 29th Jun , 2016

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Thomas Ulimwengu ambaye anaitumikia klabu ya TP Mazembe amesema Yanga bado inanafasi ya kuweza kusonga mbele katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika.

Mshambuliaji wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu

Ulimwengu amesema, bado zipo mechi nyingi kwa Yanga ambayo wakijipanga wanauwezo wa kufanya vizuri na kuendelea mbele.

Ulimwengu amesema, Yanga inakikosi kizuri ambacho kinauwezo wa kupambana na kuweza kupata ushindi mbele ya timu yoyote.

Ulimwengu amesema, wachezaji wa kitanzania wanatakiwa kutoka kwa wingi kwenda kuchezea vilabu vya nje ya nchi ili kuweza kupata wachezaji wengi wa kimataifa.