Waziri Mkuu aahidi ukarabati wa Lindi Sekondari
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaahidi Walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lindi kwamba Serikali itahakikisha miundombinu iliyoungua moto inakarabatiwa kwa haraka ili shughuli za masomo ziweze kuendelea kama awali.
