Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga
Kamanda Mpinga ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano maalumu na kituo cha redio cha EA Radio katika kipindi cha EADRIVE.
''Kwa mfano ile ajali ya City Boy kugongana kule Singida dereva alikuwa spidi ya kilomita 122 kwa saa kwa mujibu wa sheria faini ni elfu 30 na bado akaendelea na spidi baada ya kuwavuka askari, kwa wenzetu ulaya kadri spidi inavyoongezeka utatozwa faini kulingana na spidi.'' amesema kamanda Mpinga-Kamanda
Kamanda Mpinga ameongeza kuwa ''Jambo hili wote katika vyombo vinavyohusika tumependekeza kwa wanaohusika watatakiwa kulipa faini kulingana na spidi ambayo dereva alikuwa anatumia''
Kuhusu matumizi ya tochi barabarani Kamanda amesema ''Tunapoweka tochi barabarani hatupimi mabasi peke yake magari yote yatakayo pita kwa mwendo kasi yatakamatwa na kuna hadi mikoa mingine hadi pikipiki zinazokimbia mwendo hatarishi na tochi ikiziona zinakamatwa pia ''.
