Vijana wengi wana ajira zisizokidhi mahitaji yao
Leo ikiwa ni siku ya ujuzi kwa vijana duniani , Shirika la kazi duniani ILO limesema licha ya takwimu za ajira kwa vijana kuongezeka, wasiwasi umesalia juu ya idadi ya vijana ambao wana kazi lakini ni masikini.
