Friday , 15th Jul , 2016

Leo ikiwa ni siku ya ujuzi kwa vijana duniani , Shirika la kazi duniani ILO limesema licha ya takwimu za ajira kwa vijana kuongezeka, wasiwasi umesalia juu ya idadi ya vijana ambao wana kazi lakini ni masikini.

Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama

Katika mkutano wa kimataifa kuhusu kazi hivi karibuni ILO imejadlili hadhi za kazi kwa vijana mbalimbali ambapo Mtaalamu wa ajira katika ILO Sera Elda anasema Vijana milioni 235 hususani katika nchi zinazoendelea wanafanya kazi lakini katika ujira mdogo.

Amesema vijana wengi masikini ndio wanaofanya kazi ngumu za kutumia ujuzi wao lakini wanakosa nafasi ya kuweza kujikwamua kiuchumi kutokana na malipo wanayoyapata.

Takwimu zinaonyesha kuwa wakati wa mkwamo wa kiuchumi duniani vijana bilioni moja na laki mbili kote duniani walio kati ya umri wa miaka 15 hadi 24 walikuwa hawana ajira.