Makamu mwenyekiti NCCR Mageuzi avuliwa uanachama
Mwenyekiti wa chama cha siasa NCCR Mageuzi James Mbatia amesema chama hicho kimemsimamisha uongozi wa umakamu mwenyekiti (Bara) Leticia Ghati Mosore na kisha kumvua uanachama baada ya kubainika kuwa na makosa mbalimbali ya kinidhamu.

