Mmoja afariki kwa kunywa gongo Jijini Mwanza
Mtu mmoja katika kijiji cha Kitumba tarafa ya Sanjo wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza, aliyejulikana kwa jina la Wilson Magola amefariki dunia baada ya kunywa pombe aina ya gongo pamoja na pombe ya ndizi (banana) kupita kiasi bila ya kula chakula.