TPA Mtwara yakanusha kushindwa kusafirisha mizigo
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) mkoa wa Mtwara imekanusha taarifa zilizoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa bandari hiyo imezidiwa na kushindwa kumudu kusafirisha kikamilifu zao la korosho.