Rais Magufuli amlilia Mzee Kingunge
Rais Dkt. John Magufuli amepokea kwa huzuni na masikitiko taarifa za kifo cha mmoja wa waasisi wa Taifa na mwanasiasa mkongwe nchini Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kilichotokea alfajiri ya leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili.