Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam ACP Jumanne Muliro
Katika chanel hiyo ya mtandao mtuhumiwa huyo aliandika “BREAKING NEWS HUZUNI YATANDA MAZISHI YA MWAKYEMBE” taarifa ambazo ziliibua taharuki kubwa kwa wananchi hasa kwa Dkt Mwakyembe mwenyewe na familia yake.
Katika hatua nyingine Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Innocent Adam Chengula, Mhehe, 23, mkazi wa Kigogo Luanga, amekamatwa kwa tuhuma za kujinasabisha kuwa yeye ni Dkt. HASSAN ABBAS Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mtandao na kutumia laini za simu zenye usajili usio na majina yake.
Mtuhumiwa huyu amekuwa akiweka picha na majina ya Dkt. Hassan Abbas katika maelezo ya ukurasa wake mitandaoni ya kijamii (Profile) na kutuma jumbe kwa watu akiwaomba wamtumie fedha kwenye namba tofauti za simu.