Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto
Wakizungumzia adha wanazokutana nazo wananchi hao wanasema maisha yao yako hatarini kutokana na usalama mdogo wa kuvuka mto huo huku wanafunzi wa shule za sekondari wakilazimika kupanga nyumba za kuishi kijijini kuepuka gharama za kuvuka mtoni hapo.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) wilaya ya Momba Mhandisi, Selemani Mkopi amesema kuwa serikali imetupia jicho kadhia hiyo na kutenga fedha kiasi cha Tsh Bi. l2 kwaajili ya ujenzi wa daraja hilo uliotarajia kuanza mwezi wa tisa mwaka jana na kukwamishwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.