Akizungumza leo wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema serikali inaridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa mradi huo huku ikiwa mbioni kuanzisha mchakato wa ujenzi wa barabara ya haraka itakayo jengwa kwa ubiya na sekta binafsi ambapo baada ya kukamilika watumiaji watatakiwa kulipia ili kuitumia.
Kuhusu upanuzi wa ujenzi wa barabara za njia nane kutoka Kimara mwisho hadi Ubungo Kasekenya amesema wana mpango wa kujenga barabara hizo ili kupunguza msongamano kutoka eneo la Kimara hadi ubungo
Kwa upande wake Mhandisi mkazi wa mradi kutoka TANROADs Mwanaisha Rajabu amesema mradi huo unaendelea kwa kasi kubwa huku hatua za awali zikiwa zimekamilika ikisalia hatua za pili ikiwemo ujenzi wa madaraja .uwekaji taa barabarani pa moja na ujenzi wa barabara za kutoka na kuzunguka kituo cha mabasi cha magufuli licha ya kuwa changamoto imekuwa ni wananchi kutotumia vivuko vya kuvukia maalum katika njia hizo nane.