Thursday , 23rd May , 2024

Watu 11 wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa, baada ya mabomba yanayosafirisha mvuke kupasuka maungio yake katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha Mtibwa mkoani Morogoro.

Kiwanda cha sukari Mtibwa

Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Alex Mkama, amethibitisha na kusema kwamba chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika na kwamba mitambo imeharibika kwani ndiyo walikuwa wanataka kazi ya uzalishaji wa sukari.