Msanii wa BongoFleva MB Dogg
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital MB Dog amesema "Wasanii zamani kutokuwa na nguvu kwenye mitandao ya kijamii inatokana na utamaduni kwa sababu walivyokuwa wanafanya muziki walikuwa wanategemea Radio na TV na sio Facebook, Whatsapp, Youtube au Instagram, lakini sasa hivi muziki ndiyo umehamia huko kwa hiyo inawakwaza kwa wasanii wa zamani"
Aidha ameendelea kusema muziki umekuwa biashara hivyo unahitajika uwekezaji mkubwa kama pesa na sapoti, pia vitu hivyo ndiyo vimekuwa changamoto kwake hadi kumfanya kukaa kimya.
Zaidi mtazame hapa chini kwenye video.