Rapa Nikki wa Pili
Nikki wa Pili alisema haya kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instgram na kusema wasanii wengi ambao wamesainiwa chini la kampuni hizo wengi wao wameshuka kimuziki ukilinganisha na kipindi ambacho walisimama wao kama wao.
"Afrika Kusini na Nigeria muziki wao wameukuza na kuutangaza wenyewe...toka enzi za P Square mpaka Wizkid, au toka Marium Makeba mpaka Mafikizolo. ujio wa wageni ndiyo unakuja kuushusha. Mtazame Davido toka amesainiwa na Sony na kabla ya hapo...au Keko wa Uganda, au Rose Mhando..hawa walisainiwa Sony...na pili makampuni hayo lengo ni kufungua milango ya huku kwa muziki wa nje...ndiyo maana Mtv Awards main artist alikuwa Future" alisema Nikki wa Pili