Macron akutana na Xi Jinping Beijing
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekutana na Rais wa China Xi Jinping jijini Beijing, katika ziara ya siku tatu yenye lengo la kusisitiza juhudi za kusitisha vita nchini Ukraine na kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.

