Utekelezaji gridi ya taifa ya maji washika kasi
Serikali inaendelea kutekeleza kwa kasi mpango wa Gridi ya Taifa ya Maji kupitia miradi mbalimbali ya ujenzi wa maji inayotekelezwa katika maeneo yote nchini. Miradi hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama kwa uhakika na kwa muda mrefu.

