Yanga yalaani Mangungu kufanyiwa fujo na mashabiki
Uongozi wa Klabu ya Yanga umetoa pole na kulaani vikali kitendo cha vurugu kilichofanywa na baadhi ya mashabiki dhidi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu, kufuatia mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na ES Tunis ya Tunisia iliyochezwa jana, Jumapili Februari 1.

