Mbappe aifikia rekodi ya Ronaldo Real Madrid
Kylian Mbappe ameifikia rekodi ya Cristiano Ronaldo ya kufunga magoli 33 katika msimu wake wa kwanza akiwa Real Madrid baada ya kufunga magoli mawili katika ushindi wa 3-2 wa timu yake dhidi ya Leganes hapo jana katika Uwanja wa Bernabeu.