SUMATRA yasisitiza mabasi kupulizwa dawa ya mbu
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini, SUMATRA Kanda ya Mashariki nchini Tanzania imezitaka kampuni zinazotoa huduma ya usafiri kuelekea mikoani na nchi za jirani kutokea Dar-es-Salaam kutii agizo la mabasi yote kupulizwa dawa kuua mbu.

