Watanzania waadhimisha miaka 50 ya Muungano
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaongoza Watanzania katika maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.