Serikali yawasilisha bajeti kuu kwa mwaka ujao

Waziri wa fedha na uchumi wa Tanzania Bi. Saada Mkuya Salum.

Bajeti Kuu ya serikali ya Tanzania ya Sh. Tr. 19.87, imewasilishwa jana Bungeni na waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, huku ikiwabana wananchi katika bidhaa za huduma za starehe, na kipaumbele kikubwa kikiwa Elimu ikiwa na tril 3.5.

Aidha katika Bajeti hiyo, badala ya serikali kupata fedha kutoza kodi bidhaa za muhimu kwa wananchi kama mafuta, safari hii wananchi hawajaguswa katika huduma na bidhaa muhimu kwao, na badala yake fedha nyingi zinatarajiwa kukusanywa baada ya kufuta misamaha ya kodi.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS