Jaguar ajitolea kutumbuiza watoto
Jaguar, msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, ameendelea kuonyesha moyo wake wa upendo kwa jamii, safari hii akiwa amejitolea muda wake kukutana na watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo na kufurahia wakati mzuri pamoja nao.

