Ukosefu wa wataalam kikwazo sekta ya utalii Afrika
Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania Bw. Selestini Gisimba amesema sekta ya utalii hapa nchini na katika nchi za Afrika inakabiliwa na ukosefu wa wataalam licha ya kutangazwa kwa vivutio vya utalii vilivyopo katika nchi.