JK aiomba India kusaidia ujenzi wa reli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameiomba Serikali ya India kukubali kugharamia ujenzi wa reli katika Jiji laDar es Salaam ili kupunguza misongamano mikubwa ya magari na kuongeza usanisi wa usafiri.
