Wakazi wa Chato wakabiliwa na janga la njaa
Wananchi wa kijiji cha Budili wilayani Chato mkoani Geita wanakabiliwa na janga la njaa kufuatia zao la muhogo linalotegemewa kwa chakula kushambuliwa na ugonjwa hatari wa batobato michirizi kahawiya na kusababisha wengi wao kukosa chakula.