Dude hatosahau 'Macho Mekundu'
Mwigizaji Kulwa Kikumba maarufu zaidi kama Dude ameweka rekodi yake wazi kuwa tangu ameanza kufanya muvi mpaka sasa, amekwishakamilisha idadi ya muvi 75, huku filamu moja tu ikiwa katika kumbukumbu zake kama kazi bora ya wakati wote kuwahi kufanya.