Wakiongea wakati wa zoezi la ukarabati wa miundombinu itakayotumika katika michuano hiyo msimamizi wa michuano hiyo Salum Mvita na captain wa tennis katika klabu ya Gymkhana Sunjay Choksh, wamesema michuano hiyo itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na uwepo wa wachezaji nyota kutoka nje ya nchi kama Uganda, Kenya, Burundi, Rwanda na Zambia.
Aidha wamesema kuwa safari hii wanataraji kupokea idadi kubwa ya wachezaji toka nchi mbalimbali wakiwemo wa Tanzania kwa ujumla hasa ikizingatiwa katika zawadi za washindi msimu huu pia kila mshindi atapata medali na pesa taslimu kulingana na hatua aliyofika na ushindi aliopata.
Kwamujibu wa ratiba yao michuano hiyo itakua ya siku nne ikianza kutimua vumbi Juni 24 mwaka huu hadi Juni 27 ndio itafungwa rasmi na washindi kutunukiwa zawadi zao katika nafasi mbalimbali za ushindi kuanzia michezo ya mmoja mmoja na ya wawili wawili kwa jinsia zote ambao watakua wamechuana katika makundi ya umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.