Jumamosi , 13th Jun , 2015

Wananchi wa kijiji cha Budili wilayani Chato mkoani Geita wanakabiliwa na janga la njaa kufuatia zao la muhogo linalotegemewa kwa chakula kushambuliwa na ugonjwa hatari wa batobato michirizi kahawiya na kusababisha wengi wao kukosa chakula.

Wananchi wa kijiji cha Budili wilayani Chato mkoani Geita wanakabiliwa na janga la njaa kufuatia zao la muhogo linalotegemewa kwa chakula kushambuliwa na ugonjwa hatari wa batobato michirizi kahawiya na kusababisha wengi wao kukosa chakula.

Wakizungumza na EATV katika kijiji hicho wananchi hao wamesema tatizo la njaa kwao sasa limekuwa sugu kutokana na zao la muhogo ambalo ndilo tegemeo la chakula kwa wakazi wa wilaya ya Chato kushambuliwa na ugonjwa hatari wa batobato michirizi kahawia ambapo wamesema hali hiyo sasa imesababisha wakazi wengi kupata mlo mmoja kwa siku.

Kufuatia kuendelea kwa hali hiyo katika kijiji hicho jopo la wataalamu wa utafiti wa mazao kutoka katika kituo cha utafiti wa kilimo Almaruku kilichopo Bukoba kupitia wa mradi unaofadiliwa na shirika la kilimo la Bill Gate Foundation la marekani wamelazimika kupeleka mbegu mpya za mihogo ambazo zinahimili ugonjwa wa batobato michirizi kahawiaya.

Mkuu wa utafiti kutoka katika kituo cha utafi Maruku Innocenti Ndetabura amesema zoezi hilo limekuwa likienda sambamba na kutoa elimu kwa wakulima kung’oa mihogo iliyoshambuliwa na magonjwa na kupanda mbegu mpya za kisasa zisizo shambuliwa na magonjwa.

Akiongea mara baada ya kutembelea shamba la mfano ambalo limepandwa mihogo inayohimili ugonjwa wa batobato michirizi kahawia mkuu wa wilaya ya Chato Rodrick Lazaro mpogoro amewataka wakulima kusikiliza maagizo ya wataalamu.

Lazaro pia ametoa agizo kwa kila mkulima kung’oa mihogo iliyoshambuliwa na ugonjwa ili waweze kuondokana na tatizo la njaa linalo wakabili na kwamba mkulima yeyote ambaye hataondoa mihogo iliyoshambuliwa na ugonjwa huo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.