Wakulima waonywa kusaini mikataba ya Kingereza
Wakulima wa mpunga wilayani kyela wameonywa kutokubali kusaini mikataba ambayo imeandikwa kwa lugha ya kiingereza ili kuepuka ulaghai wa wafanyabiashara wanaotaka kuwaletea pembejeo za kilimo ili baadaye wanunue mazao yao kwa bei ya chini.

