Jumamosi , 5th Sep , 2015

Wakulima wa mpunga wilayani kyela wameonywa kutokubali kusaini mikataba ambayo imeandikwa kwa lugha ya kiingereza ili kuepuka ulaghai wa wafanyabiashara wanaotaka kuwaletea pembejeo za kilimo ili baadaye wanunue mazao yao kwa bei ya chini.

Mpunga ukiwa umestawi katika mashamba

Onyo hilo limetolewa na kampuni ya mtenda kyela rice ambayo imeteuliwa na serikali kupitia mradi wa uendelezaji wa kilimo kusini mwa Tanzania, sagcot, ili kuwawezesha wakulima kuzalisha mazao mengi na yenye ubora.

Kaimu afisa kilimo wa wilaya ya Kyela, Arnod Bachubila amewataka wakulima wa mpunga kutumia vema fursa hiyo ambayo imetolewa na serikali kwa ajili ya kuwainua, huku akiwataka kujifunza njia bora za kilimo kupitia mradi huo…

Hata hivyo wakulima hao wa mpunga wamelalamikia utendaji mbovu wa serikali katika usambazaji wa vocha za ruzuku ya pembejeo kuwa mara nyingi haziwafikii walengwa.