Mapigano yaibuka tena mkoani Morogoro
Mapigano yameibuka tena katika kijiji cha Tindigai ‘B’ wilaya ya Kilosa, Morogoro ambapo wakulima 11 wakiwemo mwenyekiti wa kijiji hicho na mwenyekiti wa kitongoji wamevamiwa na kupigwa na wafugaji na kupelekea kulazwa katika hospitali ya Kilosa.