Aunt Ezekiel: Tunajenga kwanza ndani ndio tutoke
Kutokana na kusuasua kwa hatua za tasnia ya filamu Bongo kuingia katika soko la kimataifa, nyota wa filamu Aunt Ezekiel amesema kuwa zipo jitihada zinafanyika sasa kuweka mambo sawa katika soko la ndani ambalo limeshuka, kama msingi wa safari hiyo.

