TPDC kusambaza gesi majumbani na kwenye magari
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema lipo kwenye mchakato wa ujenzi wa mradi wa usambazaji wa gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya majumbani, viwandani na kwenye magari katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

