Vyama 9 vyajitoa uchaguzi Zanzibar
Vyama 9 vya siasa visiwani Zanzibar vimethibitisha kutoshiriki kwenye uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika Machi 20 mwaka huu kwa kile walichokidai kuwa ni ukiukwaji wa Demokrasia unaoendelea visiwani humo.
Wakiongea leo Jijini Dar es Salaam baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa Zanzibar wamesema kuwa hawakuridhishwa na tume yua uchaguzi Zanzibar ZEC kurudia uchaguzi huo kwani hakukuwa na sababu za msingi za kurudia uchaguzi huo

