Wafanyabiashara DRC walia na vikwazo Tanzania
Umoja wa Wafanyabiashara kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini Tanzania wameiomba serikali yao kufanya mazungumzo na serikali ya Tanzania kuona ni kwa namna gani wataondoa vikwazo vinavyowakabili wakati wa kuingiza na kutoa mizigo nchini.

