Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Wa pili kushoto) akiwa katika kiwanda cha magodoro, cha Dodoma, kulia kwake ni Bw. Haidary Gulamali na kushoto ni Waziri wa Sera, Jenista Mhagama
Mkurugenzi wa kiwanda cha magodoro cha Dodoma Asili Bw. Haidary Gulamali amesema atawaleta madaktari bingwa 14 kuja kufanya upasuaji wa moyo bure kwa watoto watakaobainika kuwa na matatizo hayo.