Simba na Yanga zafungiwa kutumia uwanja wa Taifa
Serikali imezifungia timu za Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa muda usiojulikana kutokana na uharibifu wa miundombinu uliofanywa na mashabiki wa timu hizo katika mchezo wa jana.