Wasira awaonya wabunge wasiotimiza majukumu
Wakati Bunge likitarajiwa kuvunjwa Juni 27, mwaka huu, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema wabunge ambao hawakufanya vizuri katika majimbo yao wala kurudi kwa wananchi watambue chama hakitakuwa na namna ya kuwasaidia kwa sababu walipewa nafasi wakashindwa kuzitumia.