'Watanzania fugeni wanyamapori' - Rais Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Watanzania wengi zaidi kujitokeza kufuga wanyamapori kupitia bustani za wanyama (Zoo), ili kuongeza idadi ya wanyama hao na hivyo kupanua fursa za utalii na ajira.