Waziri Mkuu apongeza ujenzi wa hotel ya Bil 19.55
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema mradi wa ujenzi wa hoteli ya Golden Tulip Airport Zanzibar ni muhimu katika kuimarisha sekta ya utalii na huduma za malazi kwa wageni, wanaotumia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.