"Nitabaki CHADEMA kumalizia muda" - Mwambe
Mbunge wa Ndanda kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Cecil Mwambe, amesema kuwa kwa sasa amerejea Bungeni rasmi kumalizia muda wake wa Ubunge kwa kipindi kilichobaki na kwamba yeye ni mwanachama halali wa CCM, hivyo uchaguzi ujao atagombea kupitia tiketi ya CCM.