Mbunge wa CHADEMA aliyehamia CCM ajivunia Magufuli
Mbunge wa Viti Maalumu Anna Joram Gidarya ambaye amehama CHADEMA na kujiunga na CCM leo Juni 25, 2020 amefika katika ofisi za CCM Wilaya ya Babati mkoani Manyara na kuchukua kadi ya CCM pamoja na kula kiapo rasmi kuanza kukitumikia chama hicho.