Wabunge wawili wa CCM mikononi mwa TAKUKURU
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Dodoma imekiri kuwaita na kuwahoji Wabunge wawili wastaafu wa Chama cha Mapinduzi, akiwemo Livingstone Lusinde 'Kibajaji' ambaye ilimhoji jana na Peter Serukamba ambaye bado inamshikiliwa kwa tuhuma za rushwa.

