Sababu za viongozi Arusha kung'olewa zatajwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amezitaja sababu zilizopelekea kuwang'oa wote kwa pamoja viongozi wa Jiji la Arusha akiwemo RC, DC na DED ni kwa sababu wao walishindwa kufanya kazi kwa ushirikiano na upendo, badala yake walikuwa na malumbano yasiyo na tija.