DAS Handeni afariki Dunia kwa ajali ya gari
Aliyekuwa Katibu Tawala (DAS) Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Boniface Maiga amepoteza maisha katika ajali huku watu watatu wakijeruhiwa akiwemo Mbunge wa jimbo la Handeni Omary Kigoda ambaye amevunjika vidole viwili vya mkono wa kulia wakati wakielekea kwenye mkutano mkuu jijini Dodoma.

