Jumamosi , 18th Apr , 2015

Rapa Mabeste ambaye wiki hii aliamua kuweka wazi kuhusiana na kuuguliwa kwa mkewe, tatizo ambalo amekuwa akikabiliana nalo kwa zaidi ya miaka miwili sasa, ameleza namna mashabiki, wadau na watu wake wa karibu walivyoupokea ujumbe wake mzito.

Lisa na Mabeste

Staa huyo wa michano, ameshukuru wote ambao mpaka sasa wameweza kuwasiliana naye, kusaidia na vile vile kuzungumza naye kumpa moyo, akisisitiza pia uhitaji wa pesa za matibabu ya mkewe, na vilevile ushauri wa kitaalam ambao pia ni kati ya vitu anavyohitaji sana kwa sasa ili kusonga mbele.

Mabeste pia akatumia nafasi hii, kufafanua juu ya taarifa za ndugu wa mkewe kuchukizwa na kitendo chake cha kutangaza juu ya tatizo hilo analokabiliana nalo kwa sasa na kusema kuwa, hiyo siyo sahihi kutokana, hatua yake ikichangiwa na kuona kwa upande wao hakuna na utayari wala ushirikiano wa kutoa msaada pale ulipohitajika, mpaka yeye kufikia mahali na kuona imetosha na kuweza kuzungumza na mashabiki wake na watanzania kwa ujumla.

Mabeste