Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu akizungumza na wananchi
likiwa ni kupunguza tatizo la upungufu wa watumishi nchini.
Sangu ameyasema hayo leo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika vijiji vya Kitete, Laela, Kamsamba na Kavifuti vilivyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipouteliwa kushika wadhifa huo.
Akizungumzia nafasi za ajira ya ualimu ambazo tayari zimeshatangazwa na sekretarieti ya ajira kwenye ngazi ya mikoa kulingana na mahitaji ya mkoa husika, Mhe. Sangu amesema utaratibu wa kuwapata walimu kwa mwaka huu umeanza kuwa wa tofauti ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Amefafanua kuwa usaili huo umeanza kufanyika kwa kada ya ualimu kwa sababu nafasi za ajira za ualimu ni chache ukilinganisha na idadi ya walimu wa shule ya msingi na sekondari waliohitimu vyuo mbalimbali hapa nchini ambapo zaidi ya walimu100,000 wapo mtaani wakiwa hawana ajira.
Amesema Serikali imekuja na uamuzi huo ili kuchagiza dhana ya ushindani kwa lengo la kuhakikisha kila mwenye sifa stahiki anapata ajira katika mazingira aliyopo pasipo kulazimika kusafiri kwenda Dodoma au Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya usaili.
Kufuatia hatua hiyo Mhe. Sangu ametoa wito kwa vijana waliohitimu vyuo mbalimbali hapa nchini kuchangamkia nafasi hizo za ajira huku akiwataka wajiandae ipasavyo kwa ajili ya usaili huo, ikiwa ni mara ya kwanza kwa kada hiyo ya ualimu kufanya usaili