Jumatano , 29th Oct , 2025

Mkuu wa Kilimanjaro Mhe, Nurdin Hassan Babu ameongoza wananchi wa mkoa huo kuanza zoezi la kupiga kura katika kituo cha Kilimanjaro kikiwa ni miongoni mwa vituo 1153 kwa mkoa mzima.

Mhe, Nurdin Hassan Babu

Baada ya kupiga amewashukuru wakazi wa Mkoa huo waliojitokeza kwa wingi kupiga kura na kutimiza haki yao muhimu ya kupiga kura na kuwataka ambao bado hawajafika kwenye kupiga kura waendelee kujitokeza.

Pia, amewahakikishia wakazi wa Kilimanjaro kuwa na usalama wa kutosha na wasiwe na wasiwasi wowote usalama upo wa kutosha, wasisikilize maneno ya watu wanaosema kuwa hakuna uchaguzi