
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 61 alidhaniwa kuwa bosi wa Cosa Nostra Mafia na alikaa miaka 30 kabla ya kukamatwa mwezi Januari.
Alikuwa akitibiwa saratani wakati wa kukamatwa kwake na alihamishwa kutoka gerezani hadi hospitali mwezi uliopita.
Denaro alidaiwa kuhusika na mauaji kadhaa. Alishtakiwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2002 kwa makosa ya uhalifu ikiwa ni pamoja na kuhusika katika mauaji ya mwaka 1992 ya waendesha mashitaka wa kupambana na Mafia Giovanni Falcone na Paolo Borsellino na mara moja akajigamba kuwa anaweza "kujaza makaburi" na waathirika wake.
Pia alisimamia ulanguzi, utupaji wa taka haramu, ulanguzi wa fedha na usafirishaji wa madawa ya kulevya.
Ingawa alikuwa mkimbizi tangu 1993, Messina Denaro alidhaniwa kuwa bado alikuwa akitoa amri kwa wasaidizi wake kutoka maeneo mbalimbali ya siri.